Wednesday , 16th Dec , 2015

Msanii Linex amesema pamoja na kwamba wasanii wengi wanatoa nyimbo mpya kwa ajili ya kufungia mwaka kama zawadi kwa mashabiki wao, yeye hana mpango wa kufanya hivyo.

Linex ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba jambo hilo halikuwa kwenye mipango yake.

“Hayo mambo sijui ya funga mwaka kwamba lazima mpaka mwisho wa mwaka mi nitoe wimbo mi siamini hiyo kitu, kwa sababu haikuwa kwenye target ya muziki wangu, inawezekana labda next year nikafanya kitu kama hicho lakini kwa mwaka huu haikuwa target ya muziki wangu”, alisema Linex

Pamoja na hayo Linex ambaye ni mkali wa kuimba amesema sasa hivi ana plan za kufanya muziki wa aina mbili ambao utafanya vizuri ndani na utakaofanya vizuri nje ya nchi, baada ya kuona wasanii wengine wa Afrika wanafanya hivyo.

“Plan yangu ni kufanya game mbili, nimeona wasanii wengi wa Afrika wanafanya game mbili tofauti, yani kuna baadhi ya ngoma ukizisikia wanazofanya ni ngoma ambazo zinahit huku kwetu, zinakuwa hazisound na ngoma ambazo wanafanya kwa ajili ya jamii yao ya ndani, means na mimi ninachotakiwa kufanya napaswa na mimi pia kufanya game mbili”,

Linex aliendelea kusema kwamba pamoja na kufikiria kufanya muziki utakaokidhi viwango vya kimataifa, hawezi kuacha kufanya muziki ambao unawalenga watu wa hapa nyumbani.

“Kwa sababu siwezi kuconcetrate kwenye game ya nje wakati ndani haiwezekani, wakati ndani ndo pamesababisha mpaka nikawa na uwezo nikafikia point nikapanuka mawazo kwamba nifight kwa ajili ya game ya nje pia”, alisema Linex.

Linex pia amesema kwamba kazi yake ijayo watu watarajie kuona mabadiliko makubwa, kuanzia kwenye uimbaji mpaka kwenye video zake.