Friday , 11th Dec , 2015

Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini Tanzania (TAHLISO) limesema kuwa limefurahishwa na hali ya upatikanaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015-2016

Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini Tanzania (TAHLISO) limesema kuwa limefurahishwa na hali ya upatikanaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015-2016 ambapo asilimia kubwa ya wenye sifa za kupata mikopo hiyo wamepata kwa wakati.

Mwenyekiti wa TAHLISO Bw. Nzilanyingi Fransisco ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam na kubainisha kuwa ukilinganisha na mwaka jana kwa mwaka huu kuna ongezeko la wanafunzi elfu 18 waliopata mikopo tofauti na mwaka wa jana.

Bajeti iliyotumika kwa ajili ya mikopo kwa mwaka huu wa masomoni ni shilingi bilioni 473 bajeti ambayo ni ongezeko la shilingi bilioni 132 ikilinganisha na bajeti ya mwaka wa jana ambayo ilikuwa shilingi bilioni 341.