Monday , 23rd Nov , 2015

Diwani wa kata ya Kilungule Said Fella aka Mkubwa Fella hivi sasa anaendelea kutoa sapoti yake kwa kuendelea kufufua vipaji vya wasanii wa muziki ambapo ameelekeza nguvu zake kisiwani Zanzibar kuinua viapaji hivyo.

Msanii wa muziki Berry Black ambaye hivi sasa yupo chini ya kituo cha Mkubwa na Wanawe

Fella ambaye pia ni meneja wa kituo cha Mkubwa na Wanawe ameiambia enewz kuwa amepata mapokezi mazuri kutoka kwa wadau na mashabiki mbalimbali kwa kuinua vipaji vya chipukizi hao ambapo hivi sasa tayari ameanza kufanya kazi na wasanii nyota Berry Black na mwanadada Baby J kutoka Zanzibar.

Aidha, Berry Black ambaye alikuwa kimya kwa muda akijiandaaa kutoa kazi yake mpya ameiambia enewz kuwa ametoa wimbo wake mpya uliobatizwa jina 'Mtuache' ambao muda si mrefu video ya kazi hiyo itawafikia mashabiki na wadau wake.