
Joh Makini ameyasema hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kuwa si kazi rahisi msanii kufikia mafanikio, ila inahitaji moyo wa kutokata tamaa mpaka kufikia mafanikio.
“Lakini muziki kama maisha yako ni maisha kama ya watu wengine na kazi nyingine, kwamba kuna wakati mgumu, kuna mitihani, kuna wakati unatakiwa uwe mvumilivu, usikate tamaa, unatakiwa ujifunze kila siku, unapo lose kimoja unaweza ukapoteza ramani ya kokote unakoelekea”, alisema Joh Makini.
Joh Makini aliendelea kusema kuwa pamoja na changamoto hizo lakini iwapo msanii ataekeza zaidi katika kile anachokifanya na kuamini anaweza akafanikiwa mapema na kubadilisha maisha yake.
“Mtu mwingine anaona kama anaweza akafanya wimbo mmoja na akabadilisha maisha yake, na mi naamini inawezekana kama utaweka nguvu na mawazo yako yote hapo, ukajituma ukapush kazi yako, kwa sababu kuna watu wanatoa nyimbo 20, 30 bado maisha yanakuwa mabovu, lakini wanakuja kutoa wimbo ya 40 unabadilisha maisha yake yote, kwa hiyo hata wimbo mmoja ukitilia nguvu na nia, ukatanguliza juhudi na bidii zako mbele, inaweza kufanyika”, alisema Joh Makini.