Mmoja wa wafanyakazi wa Kiwanda cha Tangawizi Mamba Miamba, wilayani Same mkoani Kilimanjaro,
Hayo yamebainishwa na afisa kilimo, ushirika na umwagiliaji wilaya ya Same Bw. Majid Kabiemela wakati wa mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi ambao uliwakutanisha wataalamu na viongozi wa dini kwa lengo la kujadili njia za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Bw. Kabiemela amesema kuwa kiwango cha uzalishaji kipo chini ingawa kuna baadhi ya maeneo wanapata afadhali ya kupata mazao ikiwemo mahindi huku mahitaji ya chakula eneo yakiwa juu zaidi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika linalojihusisha na utunzaji wa mazingira wilaya ya Same la Hope, Mchungaji Elisa Mrutu amesema uharibifu wa mazingira katika msitu wa Shengena umechangia msimu wa mvua katika eneo hilo kutonyesha kwa wakati.