Rais wa BD Mwenze Kabinda amesema, wameamua kusimamisha Ligi hiyo kwasababu washiriki wengi wanatoka mikoani hivyo wametoa nafasi kwa kila mtu ambaye ni raia kuweza kushiriki zoezi la kupiga kura ambayo ni haki ya kila mwananchi.
Mwenze amesema, Ligi hiyo iliyokuwa iendelee mwishoni mwa wiki hii itaendelea hapo Novemba nne kwa ratiba ileile ambapo timu zote zitakuwa zimeshawasili ili kuendeleza ushindani katika Ligi hiyo.