Tuesday , 20th Oct , 2015

Chama cha mchezo wa Mieleka ya Ridhaa nchini AWATA kimesema kimeahirisha mashindano ya Nyerere Cup na sasa hivi wanaangalia mashindano ya Klabu Bingwa Taifa yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba mwaka huu.

Mwenyekiti wa AWATA Andrew Kapelela amesema, mashindano ya Nyerere Cup yaliyokuwa yakishirikisha nchi za Burundi, Uganda, Kenya na Congo yameahirishwa kutokana na mazingira yaliyo nje ya uwezo hivyo watapanga tarehe maalumu kwa ajili ya mashindano hayo.

Kapelela amesema, mashindano ya klabu bingwa ambayo hivi sasa yapo mbele yao yatashirikisha vilabu mbalimbali vya Tanzania ambavyo vinaamini vina uwezo wa kushiriki.