Tuesday , 13th Oct , 2015

Star wa muziki ambaye aliibukia katika dansi, Shetta Shettani ambaye pia amesimama vizuri kabisa kama moja ya majaji wa michuano ya Dance 100% 2015 kwa mwaka huu, ameeleza namna ambavyo nafasi hiyo imekuwa na umuhimu kwake.

Staa wa muziki nchini Shetta Shettani

Nyota huyo ambaye ameshuhudia juhudi za washiriki hao tokea mwanzo wa michuano hiyo amekiri kuongeza ujuzi mkubwa kwa upande wa fani yake kama msanii na kutoa pongezi kwa madensa hao waliotwaa ubingwa na kujizolea kitita cha shilingi milioni tano.

Shetta amesema kuanzia mwanzo wa mashindano hayo mpaka mwisho amepata nafasi muhimu kabisa na ya heshima kuona vipaji, kujifunza na kuamua, kauli aliyotoa pembeni ya tathmini ya namna ambavyo mashindano hayo yamekuwa na uzoefu na changamoto ya kipekee kwake na kwa niaba ya majaji wenzake.