Monday , 5th Oct , 2015

Msanii wa muziki Bebe Cool wa nchini Uganda amejikita katika shughuli ya hisani kuchanga fedha za matibabu ya mtoto mwenye tatizo kubwa la moyo anayejulikana kwa jina Israel.

Msanii wa muziki Bebe Cool wa nchini Uganda

Bebe Cool hadi sasa amefanikiwa kuendesha tukio la uoshaji magari kusaidia kupatikana kwa fedha za matibabu ya mtoto huyo ambapo baada ya kujikita kwa nguvu katika zoezi hilo, mchango wa msanii huyo umeanza kuzaa matunda hasa baada ya watu wengi kuguswa wakiwepo mastaa mbalimbali wa Uganda ambao nao wamemuunga mkono kumsapoti katika kampeni hiyo.

Star huyo amefanya zoezi hilo ikiwa pia ni kama mfano kwa wengine hususan kutoka jamii ya wale waliojaliwa kuwa na ziada, kuchukua hatua kutoa msaada, hususan katika mazingira ya sasa yaliyogubikwa na watu wanaopitia changamoto mbalimbali za kiafya na kiuchumi.