Monday , 5th Oct , 2015

Shirika la Umeme nchini Tanzania (TANESCO) limebuni mradi wa kusambaza huduma za umeme mijini ili kukabiliana na wimbi kubwa la wateja wa mijini wanaohitaji kuunganishiwa umeme.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ugavi la umeme nchini (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba

Akiongea jana usiku katika mahojiano na kituo cha TBC Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Felchesmi Mramba amesema tayari wameshafanya gharama za mradi huo na kubaini nyumba zote za mjini zinazohitaji umeme.

Mramba amesema mradi huo wa miaka mitatu umepata wadau wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) ambao wamekubali kusaidia baadhi ya mikoa.

Akizungumzia mafanikio Mramba amesema wamefanikiwa kuwaunganishia umeme wateja na kufikia asilimia 40 mwaka 2015 kutoka wateja asilimia 8 mwaka 2008.