Msemaji wa Azam FC Jaffar Maganga amesema, ligi ya safari hii ni ngumu kutokana na kila timu kuhitaji kushika nafasi ya juu ili kuweza kuipeperusha bendera ya nchi kimataifa.
Maganga amesema, Kombe la Shirikisho FA limekuwa na changamoto kubwa kwa vilabu kufanya maandalizi mazuri ili kujihakikishia inafanya vizuri katika michuano hiyo ya ligi kuu ya Soka Tanzania Bara pamoja na kombe la FA linalotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba mwaka huu.

