Wednesday , 9th Sep , 2015

Chama cha Mpira wa Magongo Mkoa wa Dar es salaam DRHA kimesema kimejipanga kwa kuhakikisha timu ya taifa inayotarajia kushiriki mashindano ya kufuzu michuano ya Olimpiki ya Afrika inashindana na sio kushiriki mashindano hayo.

Katibu Mkuu wa DRHA Mnonda Magani amesema, wanatimu mbili ya wanawake na wanaume ambapo kila timu inawachezaji 20 wakiendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano hayo ambapo timu hizo zitaelekea nchini Afrika kusini katika ya Oktoba 19 na 20 mwaka huu kwa ajili ya kufanya maandalizi ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Oktoba 24 mpaka Novemba Mosi mwaka huu nchini Afrika kusini.

Magani amesema, wanaamini jitihada za mazoezi zitaweza kuwasaidia kuweza kushinda katika mashindano hayo yanayotarajiwa kushirikisha nchi mbalimbali za Afrika zinazocheza mchezo zilizo chini ya chama cha mpira wa magongo barani Afrika AHA.