Wednesday , 2nd Sep , 2015

Msanii wa Uganda Bobi Wine ambaye kwa upande wa pili ana mapenzi na kipaji cha mchezo wa ndondi, ameonekana katika siku za karibuni akijifua kwa mazoezi makali ya mchezo huo, na kuchochea uvumi wa tetesi kuwa ana mpango wa kurejea rasmi ulingoni.

Bobi Wine

Msanii wa Uganda Bobi Wine ambaye kwa upande wa pili ana mapenzi na kipaji cha mchezo wa ndondi, ameonekana katika siku za karibuni akijifua kwa mazoezi makali ya mchezo huo, na kuchochea uvumi wa tetesi kuwa ana mpango wa kurejea rasmi ulingoni mwishoni mwa mwaka.

Star huyo amekuwa akitumia muda wake nyumbani kwake kupasha ujuzi wake wa ndondi akiwa na mwalimu ambaye hajajulikana bado ni nani, na tayari moja ya kipande cha video inayoonesha sehemu ya mazoezi yake, imekwishaanza kusambaa mitandaoni.

Taarifa hizi zinakuja ikiwa inafahamika kuwa, Bobi alikwishawahi kunyimwa nafasi na kamisheni ya mchezo wa ndondi Uganda UPBC mwaka 2008, mazoezi ya sasa yakiwa ni dalili tosha ya star huyo kujipanga kukifufua tena kipaji chake hicho.

Tags: