Friday , 28th Aug , 2015

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema itazifungwa hotel zote hata za nyota tano kama hazizingatii Kanuni za Afya kutokana na kubainika kuwa hoteli nyingi hazina mifumo maalumu ya uhifadhi maji taka na kuyatitirisha mitaani.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Donald Mbando

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Donald Mbando na kuongeza kuwa maeneo yote wanayouza chakula bila kujali hadhi yake na eneo zilizopo zitafungwa kwani tafiti zinaonesha jamii bado haifuati kanuni za Afya japo elimu ya kuzuia na kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu inatolewa kila siku.

Dkt. Mbando ameongeza kuwa idadi ya wagonjwa imeongezeka hadi wagonjwa 385 huku waliopo makambini ni wagonjwa 70 kwa Mkoa wa Dar es salaam huku mkoa wa Pwani kifo kimoja na wagonjwa 7.

Dkt. Mbando amezidi kuwakumbusha wananchi kujali kanuni za Afya wakati wote pamoja na kuweka mazingira yote katika hali ya usafi na usafi kwa mtu mmoja mmoja.

Wakati huo huo wizara ya Afya imepokea msaada wa dawa za kutibu maji toka shirika la Afya duniani ili kudhibiti ugonjwa huo na magonjwa yote ya kuambukiza.