Wednesday , 19th Aug , 2015

Msanii wa miondoko ya Bongofleva Shetta amezungumzia kuhusu video ya wimbo wake wa Shikorobo ambao umekuwa ni hit ndani na nje ya nchi uliompa nafasi kubwa ya kujitangaza zaidi kupitia kolabo aliyoifanya na nyota wa Nigeria, KCEE.

Msanii wa miondoko ya Bongofleva Shetta akiwa na mkali wa Nigeria Kcee

Shetta ambaye pia ni mmoja wa jaji wa shindano kubwa la Dance 100% mwaka huu ameongea na eNewz kuhusiana na maprodyuza walioweka mikono yao ndani ya project yake hiyo ambayo hadi kukamilika ilipewa kipau mbele na watayarishaji hao akiwemo Tudd Thomas.