msanii wa Hip hop Keko wa Uganda akiwa na msanii mwenzake Sheebah Karungi
Sheebah amelazimika kutolea ufafanuzi tetesi hizo baada ya kusambaa kwa uvumi kwa muda sasa hususan kupitia mitandao, kuwa kuna mahusiano ambayo si sawa yanaendelea kati yake na Keko.
Vilevile sambamba na hilo, Sheebah amezungumza juu ya kujipanga kufanya shoo ya kwake binafsi kama wasanii wengine wakubwa Uganda, mpango ambao amesema upo na utakamilishwa katika siku za mbeleni mambo yakikaa sawa.