Tuesday , 25th Mar , 2014

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Kangi Lugola amemuomba Mwenyekiti wa Bunge kutengua uteuzi wake wa wajumbe wa Kamati ya Uongozi ili kuondoa manung'uniko na awateuwe watu kwa kuzingatia makundi mbalimbali bila ya kuwa na mtu kutoka chama cha CCM.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta alisita kubatilisha uteuzi wake huo uliolalamikiwa kuwa umependelea zaidi wajumbe kutoka chama cha CCM, na kusema kuwa yaliyokwisha fanyika yameshafanyika, ila ataendelea kupokea ushauri wa wujumbe na atakayekataa uteuzi ana haki ya kufanya hivyo.

Kauli ya Lugola ilifuatia malalamiko ya baadhi ya wajumbe wa bunge hilo kuhusu uteuzi huo, ambayo pia yalipelekea mjumbe wa Prof. Ibrahim Lipumba kukataa uteuzi aliyopewa katika kamati ya uongozi, kufuatia wenyeviti wa Kamati zote kutokea CCM, isipokuwa Hamad Rashid wa chama cha (CUF).