Wednesday , 29th Jul , 2015

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeongeza saa kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR, Mkoani Dar es Salaam kwa kuanzia saa moja asubuhi badala ya saa mbili kama ilivyokua awali

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (Nec), Jaji mstaafu Damian Lubuva.

Akizungumza na Waandishi jijini Dar es Salaaam baada ya kukutana na wakurugenzi wa jiji la Dar es Salaam Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema wamebadilisha muda huo ili wananchi wote waweze kujiandikisha katika Daftari hilo.

Lubuva ameongeza kuwa kwa sasa tume hiyo haiwezi kuzungumza iwapo itaongeza muda wa kujiandikisha lakini itahikikisha watu wote wameandikishwa katika Daftari hilo.

Aidha Nec imesema idadi ya walioandikishwa kwenye daftari hilo hadi kufikia juzi ni watu milioni 1, laki 172, 855 ikiwa Kinondoni ni watu laki 490,228, Temeke laki 389,558 na Ilala ni laki 302,871.