Tuesday , 21st Jul , 2015

Zoezi la uchukuaji wa fomu za kuwania nafasi ya Ubunge kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Mbeya mjini linazidi kushika kasi baada ya idadi kuongezeka hadi jana kufikia watia nia 15.

Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara Ndugu Phillip Mangula.

Wakizungumza na chombo hiki kwa nyakati tofauti watia nia hao wametaja vipaumbele vyao kama ambavyo Charles Mwakipesile alivyosema kabla ya kwenda kuchukua fomu kuwa endapo chama chake kitampa ridhaa ya kupeperusha bendera atabadilisha mfumo wa ofisi ya mbunge.

George Chanda ni Mwandishi wa habari mkongwe mkoani Mbeya wa gazeti la The Guardian aliuliza swali huku akirejea historia ya wabunge nane waliotangulia ukiwaacha Benson Mpesya na mbunge aliyemaliza muda wake Joseph Mbilinyi “Sugu”.

Baada ya kutoa historia hiyo mwandishi Chanda alifuatia na swali kwa mtia nia huyo kilichomsukuma kuchukua fomu huku mtia nia huyo akijibu.

Wakati huo huo, mtia nia mwingine Samweli Mwaisumbe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua Fomu katika Ofisi za CCM wilaya ya Mbeya, maeneo ya uwanja wa Sabasaba amesema akipata ridhaa ya kuwania jimbo la Mbeya mjini ataangalia zaidi suala la ajira.

Aidha baadhi ya akina mama lishe, wananchama na wananchi wa jiji la Mbeya wakizungumza na chombo hiki wamesema Mwaisumbe anatosha kupeperusha bendera jimbo la Mbeya mjini kama ambavyo Hiba Msemwa, Chichi Mkandawile na Tainess Nkanyage wanavyosema.