Friday , 19th Jun , 2015

Baada ya Mr Blue, Byser kutangaza rasmi kuachana na matumizi ya vilevi, huku akimpa mkewe maksi zote kwa kumfanikisha kufikia hatua hiyo, star huyo wa muziki ameweka wazi kupata muitikio tofauti kutoka kwa wadau na mashabiki wanafuatilia kazi zake.

Mr Blue jukwaani

Blue amesema kuwa, wakati wengi wakiwa hawaamini kuwa anaweza kuachana na vitu kama bangi na sigara, amepokea pongezi nyingi, na kwa upande mwingine kusikia wapinzani wake wakipata hofu juu ya nguvu yake mpya akiwa sober katika gemu.

Mke na Mtoto wa Mr Blue