Monday , 15th Jun , 2015

Baada ya watu wa karibu wa msanii wa Mabeste kulalamikia hatua ya Jux kutotaja mchango wa Mabeste katika ngoma yake ya Sisikii iliyompatia tuzo, mashabiki wa Mabeste wamekuwa na maoni hasi juu yake.

Mabeste

Star wa muziki Mabeste, amekuwa na wakati mgumu kupambana na maoni hasi kutoka kwa mashabiki kufuatia hatua ya mke na meneja wake, Lisa kulalamikia hatua ya mumewe huyo kutokutajwa kama moja watu wenye mchango mkubwa kwa rekodi ya Jux ya 'Sisikii' baada ya kuchukua tuzo.

Mabeste ameweka wazi kuwa hana tatizo na Jux isipokuwa kaguswa tu kwa kutokutajwa kama moja ya mhusika mwenye mchango mkubwa kwa kazi hiyo.

Hata hivyo star huyo bado anaonesha kuguswa na hatua ya kutokupata simu ama ujumbe mfupi wa moja kwa moja kutoka kwa Jux kumshukuru kutokana na mchango wake katika kazi yake, ukiachia kutajwa tu katika mtandao wa Instagram.