Monday , 15th Jun , 2015

Kocha wa kituo cha Magolikipa nchini TGC, Manyika Peter amesema, kituo chake kipo katika mpango wa kuwapatia timu za nje magolikipa wake li kuweza kukuza zaidi vipaji vyao.

Akizungumza na East Africa Radio, Manyika amesema, Julai mwaka huu uongozi wa kituo cha kukuza vipaji vya magolikipa kilichopo nchini Rwanda watakuja kwa ajili ya kuangalia vipaji na kufanya muungano kwa ajili ya kufanya kazi pamoja.

Manyika amesema, wameamua kutafuta mawakala ambao watakuwa wakiwasiliana nao pindi watakapoona kipa yupo sawa kwa ajili ya kwenda kuchezea timu za nje ili iwe rahisi kwa kituo hicho kutoa magolikipa kwenda nje ya nchi.