Wednesday , 10th Jun , 2015

Msanii wa muziki wa nchini Uganda, Eddy Kenzo pamoja na Rema Namakula ambaye ni mama mtoto wake, wamefanikiwa kuhamia katika jumba la kifahari la msanii huyo ambalo linakadiriwa kufikia thamani ya shilingi milioni 500 za Uganda.

wasanii wa muziki wa Uganda Eddy Kenzo na Rema Namakula

Mastaa hawa pamoja na marafiki zao wiki hii wamefungua nyumba hiyo kwa maombi maalum kama ishara ya mwanzo mzuri wa hatua hii mpya aliyoipiga, ikiwa pia ni matunda ya mafanikio makubwa ambayo amevuna kutokana na muziki wake.

Rema kupitia ujumbe aliouweka mtandaoni ameonesha kufurahishwa na makazi hayo mapya ambayo ni nguvu kubwa ya baba mtoto wake, akiandika maneno yanayosomeka "God is my HERO from Nakivubo Stadium to Kenzo paris Sseguku..".