Friday , 1st Feb , 2019

Kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema katika mchezo wa jana dhidi ya Biashara United, hawezi kuilaumu timu nzima kwa mabao mawili waliyofungwa, bali ni kwa uzembe wa mchezaji mmoja mmoja.

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera

Kocha Zahera amesema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wa kombe la Shirikisho la Azam, ambapoYanga imeiondoa Biashara United kwa mikwaju ya penalti 5-4, akisisitiza kuwa wachezaji wake walikosa nafasi nyingi ambazo hawakuzitumia zilizopelea mchezo huo kufikia hatua ya mikwaju ya penalti.

"Mechi ya leo (jana) magoli tuliyofungwa, hayakuwa ni makosa ya safu ya ulinzi, bali ni makosa ya mchezaji mmoj mmoja. Mfano lile kosa ambalo Ajib amefanya, sio kosa la ulinzi bali ni kosa la yeye mchezaji na Ajib sio mlinzi", amesema.

"Sisi tumepata nafasi nyingi kushinda hata wao, tumepata nafasi tano lakini tumeshindwa kuzitumia. Makambo wa leo ni yule ambaye alikuwa anafanya vitu vya hovyo hovyo tuu, yaani tokea ameenda DR Congo wiki mbili, hivi sasa hafanyi kitu", ameongeza Zahera.

Baada ya ushindi huo, Yanga sasa inafuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo, ikiungana na baadhi ya vigogo wa ligi kuu bara Azam FC na Mbeya City .