
Katibu Mkuu wa Yanga Baraka Deusdedit amesema, wanashangaa kwanini TFF inasimia mchakato mzima wa uchaguzi wa klabu yao ilhali wao wenyewe wanakamati yao ya uchaguzi na TFF inatakiwa kubaki kama wasimamizi wa kuangalia kama Yanga haijafanya uchaguzi wachukue hatua gani.
Deusdedit amesema, kama TFF isingekuwa inautambua uongozi wa Yanga ambao bado upo madarakani isingekuwa inamuhusisha kiongozi yoyote akiwemo Makamu Mwenyekiti wa Yanga katika vikao mbalimbali vyashirikisho.
Deusdedit amesema, kwa upande wao wameamua kufanya uchaguzi mapema ili kutimiza matakwa ya serikali ikiwa ni pamoja na kupata viongozi watakaosaidia Klabu ya Yanga katika maandalizi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Deusdedit amesema, kwa pamoja rai yao ni kufanya uchaguzi Juni 11 mwaka huu ambapo kesho ambayo ni Juni 02 na 03 itakuwa ni siku ya kuchukua fomu za uchaguzi na kuzirejesha huku Juni 04 ikiwa ni siku ya kikao cha mchujo wa awali wa wagombea na kuitangaza orodha ya awali ya wagombea.
Deusdedit amesema, June 05 watakuwa wanapokea mapingamizi ya wagombea huku Juni 06 na 07 itakuwa ni siku ya kupitia pingamizi zote na kufanya usaili wa awali na kupeleka majina na TFF kuyafanyia uhakiki na kuweza kutangaza maamuzi ya kamati ambapo pia itakuwa ni siku ya kukata rufaa, kusikiliza na kutolewa maamuzi ya rufaa kazi itakayofanywa na TFF.
Deusdedit amesema, Juni 07 mpaka 10 itakuwa ni siku ya kufanya kampeni kwa wagombea ambao watakuwa wameainishwa huku Juni 11 ukifanyika uchaguzi na Juni 12 matokeo yatatoka.
Deusdedit amesema, lengo la kufanya uchaguzi huo mapema tofauti na TFF ilivyoelekeza ni ili kuweza kuweka nguvu zaidi katika mashindano ya kombe la shirikisho.
Kwa upande wa TFF imesema wanaendelea na mchakato wa uchaguzi ambapo wameongeza muda mpaka jumatatu ya Juni 06 tofauti na pale awali kama BMT ilivyotangaza kuwa mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu iwe jumapili Juni 05.
Afisa Habari wa TFF Alfredy Lucas emesema, idadi ya wanachama wa Yanga kuchukua fomu imeongezeka ambapo mpaka sasa wamefikia wanachama tisa hivyo zoezi la uchaguzi linaendelea vizuri na uchaguzi utafanyika Juni 25 kama ilivyopangwa.