Timu ya Yanga imewasili salama visiwani Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa na mahasimu zao Simba kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara Jumamosi ijayo.
Kikosi hicho cha Yanga kipo Pemba na kesho kitaanza mazoezi kwenye uwanja wa Gombani, kwa mazoezi ya siku tano hadi Jumamosi kuikabili Simba.
Yanga SC iliondoka Dar es salaam Ijumaa saa 1;00 usiku kwenda Mauritius kwa ndege ya kukodi, mara baada ya uongozi wa timu hiyo kubadili ratiba ya kwenda Jumatano kwa ndege ya abiria.
Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara waliwasili majira ya saa 4;00 asubuhi, na hadi saa 6;00 mchana, tayari walikuwa Pemba.
Yanga ilijewekea mazingira mazuri ya kuingia raundi ya pili ya michuano ya vilabu Barani Afrika, baada ya kushinda bao 1-0 ugenini dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius hapo jana, na timu hizo zitarudiana wiki mbili zijazo jijini Dar es salaam.





