Tuesday , 24th Jan , 2017

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemwondoa Mwamuzi Hussein Athuman kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi Kuu baada ya kupata alama za chini ambazo hazimwezeshi kuendelea tena kuchezesha ligi hiyo.

Mechi ya Yanga na Majimaji

 

Mwamuzi Hussein Athuman kutoka Mkoa wa Katavi alichezesha mchezo namba 150 uliozikutanisha timu za Majimaji ya Songea na Young Africans ya Dar es Salaam, kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.

Kadhalika Young Africans imepigwa faini ya jumla ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kutokana na timu yao kutoingia vyumbani, na pia kutumia mlango usio rasmi wakati wa kuingia uwanjani.

Adhabu hizo zimetolewa na TFF na kuwagusa waamuzi, wachezaji na na vilabu mbalimbali ambapo Mwamuzi Ngole Mwangole pia amepewa barua ya onyo kali baada ya kubainika kukataa bao lililoonekana kutokuwa na mushkeli la Mtibwa Sugar dhidi ya JKT Ruvu katika mechi iliyofanyika Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

Maamuz mengine yaliyotangazwa na TFF ni kuusimamisha uwanja wa Jamhuri Morogoro kutumika kwa michezo ya ligi kuu ili kutoa fursa kwa wamiliki kufanya marekebisho makubwa kwenye eneo la kuchezea (pitch).