Monday , 7th Dec , 2015

Mabingwa watetezi wa soka Tanzania Bara, Yanga wanatarajia kuweka kambi Mjini Bagamoyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya muendelezo wa michuano ya Ligi kuu inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 12 mwaka huu.

Yanga itaivaa Mgambo Shooting Desemba 12 wakati Ligi Kuu Bara itakapoanza kutimua vumbi, baada ya hapo italazimika kubaki Tanga kuivaa African Sports.

Klabu hiyo iliyo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo inaendelea na mazoezi jijini Dar es salaam ikiwa na kikosi chake kamili ambapo itakapoweka kambi Bagamoyo itakaa mpaka karibia na kuanza kwa Ligi, ndipo itasafiri kuelekea jijini Tanga.