
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Klabu ya Yanga Jerry Muro amesema, kikosi kinaweka kambi nje ya nchi kwa ajili ya kutafuta mbinu za kuweza kuwakabili Waalgeria hapo Juni 17 mwaka huu.
Muro amesema, wanaamini kambi ya nje ya nchi itaweza kuwasaidia kuleta matokeo mazuri na kupeperusha vizuri bendera ya Tanzania katika soka.
Kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kikijiandaa na mchezo wa hatua ya makundi ya Shirikisho Afrika utakaopigwa June 17 mwaka huu ambapo Yanga itaanzia ugenini nchini Algeria.