Kocha mkuu wa Watford Quique Sánchez Flores(kushoto)akiwa na nyota Odion Ighalo(kulia)kwenye picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa tuzo za kocha na mchezaji bora wa EPL kwa mwezi disemba mwaka jana.
Mshambuliaji wa klabu ya Watford Odion Ighalo na kocha wake Quique Sanchez Flores wametajwa kuwa mchezaji na kocha bora wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza kwa mwezi disemba.
Ighalo raia wa Nigeria aliifungia mabao matano mwezi disemba na kuiwezesha Watford kuzishinda klabu za Norwich City, Liverpool, Sunderland huku ikitoa sare na Chelsea na kupoteza mechi moja pekee dhidi ya Totenham Hotspurs.
Kikosi cha Flores kilizoa Pointi 10 katika Mechi zao 5 za Mwezi Novemba kwa kuzifunga Norwich, Sunderland na Liverpool na kutoka Sare na Chelsea na kupanda kuwa kwenye Timu 10 za juu kwenye Msimamo wa Ligi.
Flores raia wa Hispania amewabwaga makocha Arsène Wenger wa Arsenal, Claudio Ranieri wa Leicester City na Alan Pardew wa Newcastle United huku ighalo akiwashinda Mesut Özil wa Arsenal, Marko Arnautovic wa Stoke City, Riyad Mahre wa Leicester City, Romelu Lukaku wa Everton na Dele Alli wa Titenham Hotspurs.