Thursday , 26th Nov , 2015

Watanzania na mashabiki wa soka nchini wametakiwa kutoikatia tamaa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars baada ya kufungwa bao 7-0 na Algeria katika mchezo wa marudiano wa kuwania kupangwa katika makundi ya kushiriki kombe la dunia 2018 nchini Urusi

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick amesema, pamoja na kufungwa watanzania wanatakiwa kuendelea kuipa sapoti timu hiyo ili iweze kurekebisha makosa.

Sadick amesema, shirikisho la soka nchini TFF pia linatakiwa kuwajibika kuijenga timu upya kwa kuangalia wapi palikuwa na makosa kwani bado wachezaji ni wazuri.

Sadick amesema, TFF inatakiwa kuendeleza vijana wanaotakiwa kuendelezwa ndani ya timu ya taifa na hata wale ambao uwezo wao umeshafikia mwisho watakapoondoka wanatakiwa kuandaliwa wachezaji wengine watakaounda timu itakayokuwa madhubuti kwa miaka ijayo.