
Akizungumza na East Africa Radio, Afisa Michezo wa Baraza la michezo nchini BMT Benson Chacha, amesema, katika nafasi ya Urais watu wanne waliomba kugombea nafasi hiyo ambapo watatu ambao ni Magesa Paul Mwakabeta, John Jose Ndumbalo na Hamad Abdallah Mkombozi ambao wamepita katika nafasi zao huku Nurdin Hussein akiondolewa kwa kukosa sifa.
Chacha amesema katika nafasi ya makamu wa Rais waligombea wagombea wawili ambao ni Samuel Kafyeta na Daud Nandi ambapo kamati imewapitisha wote huku katika nafasi ya katibu mkuu wakigombea watatu ambao ni Iddy Kibwana, Mosses Mabula na Peter Sarungi ambao wamepitishwa kwa kuwa mna sifa.
Chacha amesema kwa upande wa muweka hazina waligombea watatu ambao ni Honorina Banzi, Yusuph Kosi na Ronward Alex ambao wote wamefutwa katika ugombea kwa kukosa vigezo ambapo kamati inatarajia kufanya uchaguzi mdogo wa muweka hazina baada ya kumaliza Uchaguzi wa Paralympic kutokana na nafasi hiyo kuwa wazi.
Chacha amesema nafasi wa wajumbe wa kamati ya utendaji iliwasilishwa ikiwa na wagombea 16 ambao wamepitishwa wote kutokana na kukidhi vigezo.