Friday , 17th Apr , 2015

Wanawake nchini wametakiwa kujiingiza katika masuala ya michezo hususani katika kusomea kozi za uamuzi ili kuweza kuwa waamuzi katika mechi mbalimbali za mpira wa miguu ndani na nje ya nchi.

Akizungumza jijini Dar es salaa, wakati wa kufungwa kwa kozi ya waamuzi vijana chini ya miaka 17, mwenyekiti wa Chama cha Mpira mkoani Kagera KRFA, Salim Chama amesema, katika kozi hiyo kuna waamuzi wawili wa kike kati ya 35 walioshiriki kozi hiyo, hivyo wanatakiwa kuwahamasisha vijana wenzao wa kike ili kuweza kusomea kozi ya waamuzi hapa nchini.

Chama amesema, jamii inatakiwa kuachana na tafsiri tofauti kuwa msichana akiwa muamuzi anakuwa na matendo mabaya suala ambalo siyo sahihi kwani uamuzi ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine.