Wednesday , 20th Jul , 2016

Waamuzi wa Ligi kuu nchini wametakiwa kujifanyia tathimini ya mechi za misimu iliyopita ya Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara ili kuweza kuepukana na lawama ambazo hutokea mara baada ya kumalizika kwa mchezo.

Kocha msaidizi wa Kagera Sugar Ally Jangalu amesema, waamuzi wanatakiwa kuwa makini katika kipindi cha Ligi ili kuondoa vurugu ambazo hutokana na waamuzi wa mchezo husika kufanya jambo ambalo huweza kumgharimu mwishoni mwa mchezo.

Kwa upande mwingine Jangalu amesema, kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara anaendelea kukiandaa kikozi chake kwa ajili ya kuweza kupambana zaidi ili kuweza kushinda katika mchezo wa awali ambao wataanzia nyumbani dhidi ya Mbeya City.

Jangalu amesema, wanaamini ligi itakuwa na ushindani kutokana na kila timu kujiandaa ili kuweza kupambana na ushindani wa ligi lakini kwa upande wake anaamini kutokana na maandalizi kikosi chake kitambambana ili kuweza kuhsinda mchezo wa nyumbani ambao ni muhimu pamoja na michezo mingine ili kujiweka katika nafasi nzuri katika Ligi hiyo.

Jangalu amewataka mashabiki wa Kagera Sugar kujipa imani na timu yao kwani wanaamini watafanya vizuri tofauti na misimu iliyopita.