Wednesday , 6th Jan , 2016

Viongozi wa vyama mbalimbali vya michezo nchini wameungana na kuunda umoja wa michezo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Michuano ya Olimpiki mwaka huu.

Viongozi wa vyama mbalimbali vya michezo nchini wameungana na kuunda Umoja wa michezo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Michuano ya Olimpiki mwaka huu.

Akizungumza na East Africa Radio Mwenyekiti wa Umoja huo Lukelo Wililo amesema, wameamua kuwaan Umoja huo ambao utakuwa chombo kikuu cha kuwasemea changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika michezo kwa ujumla.

Wililo amesema, umoja huo utasaidia viongozi kuwa na nguvu na kusikika pale kitakapowasilisha matatizo au suala lolote linalohusiana na michezo hapa nchini.

Wililo amesema, malengo yao kwa sasa kuelekea Olimpiki ni kujiandaa mapema na kuungana kwa pamoja ili kuweza kuandaa timu za taifa za michezo mbalimbali na kuhakikisha wanafanya maandalizi mapema maandalizi ya kuweza kufuzu michuano ya Olimpiki pamoja na ushiriki mzima wa mashindano hayo yatakayofanyika Septemba mwaka huu Rio nchini Brazil.

Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja huo ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Judo nchini JATA Innocent Malya amesema, umoja huo utakuwa na manufaa makubwa kwani utasaidia vyama mbalimbali vya michezo ambavyo mpaka sasa bado havijashiriki mashindano yoyote ya kufuzu ushiriki wa michuano ya Olimpiki mwaka huu.

Malya amesema, wapo nje ya muda hivyo umoja huo utakuwa na uwezo wa kuweza kusaidia kutafuta wadau na serikali kwa ajili ya kuweza kudhamini vyama hivyo.