Tuesday , 15th Jan , 2019

Mtendaji Mkuu wa kamati ya ndani (Local Organizing Commitee), inayosimamia maandalizi ya michuano ya AFCON U17 inayotarajiwa kufanyika nchini mwaka huu, Leslie Liunda, amesema maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo yapo katika hatua nzuri.

Uwanja wa taifa.

Liunda ameweka wazi kuwa tayari awamu ya kwanza ya ukaguzi kutoka kwa kamati maalum ya shirikisho la soka Afrika (CAF), umeshafanyika na wametoa maelekezo juu ya nini cha kufanya kuelekea michuano hiyo.

''Vitu vinavyohitajika katika kufanikisha michuano hii kama viwanja vya mechi na mazoezi, hoteli na hospitali vyote vimekaguliwa katika awamu ya kwanza hivyo tunaendelea kufanyia kazi maelekezo yaliyotolewa'', amesema.

Pia ameweka wazi kuwa viongozi hao wa CAF walitaka kusikia serikali inasema nini kuelekea michuano hiyo ambapo Waziri Mkuu Kassim Maliwa pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe waliwahakikishia kuwa serikali ipo tayari kwa michuano hiyo.

Viwanja ambavyo vimepnagwa kutumika katika michuano hiyo ni Uwanja wa Taifa, Uwanja wa Uhuru na Uwanja wa Chamanzi.

Jumla ya timu 8 ikiwemo mwenyeji Tanzania zitashiriki michuano hiyo. Mataifa mengine ni  Morocco, Senega, Guinea, Nigeria, Cameroon, Uganda na Angola. Michuano itaanza April 14 na kumalizika April 28, 2019.