Friday , 1st Jan , 2016

Ligi Daraja la Daraja la Kwanza ambayo washindi wake wa kwanza kutoka kila kundi watakwea kucheza ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu ujao inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo kumi na mbili kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini.

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi nchini Boniface Wambura akizungumza na waandishi wa habari

Katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam Ashanti United itaumana na Polisi Dodoma, Polisi Morogoro watawakaribisha Kurugenzi FC ya Mafinga katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, huku Kimondo FC wakicheza dhidi ya Burkinafaso kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Maafande wa Ruvu Shooting watacheza dhidi ya Mji Njombe katika uwanja wa Mabatini Mlandizi, Lipuli dhidi ya JKT Mlale katika uwanja wa Wambie mkoani Iringa, maafande wa JKT Kanembwa wakiwakaribisha Mbao FC katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Geita Gold watawakaribisha Polisi Mara kwenye uwanja wa shule ya Nyankumbu mjini Geita, JKT Oljoro watacheza dhidi ya Rhino Rangers uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, huku maafande wa Polisi Tabora wakiwakaribisha Panone FC katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Siku ya Jumapili Africa Lyon itaumana na ya Kiluvya United kwenye uwanja wa Karume, huku timu ya Kinondoni Municipal Council (KMC) wakicheza dhidi ya Friends Rangers katika uwanja wa Mlandizi Mabatini.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>