Wane Mkisi ambaye ni kocha wa mpira wa miguu nchini amesema, soka linatakiwa kuanza kukua kuanzia chini na watanzania wanatakiwa kuwa wavumilivu ili kuweza kupata matokeo mazuri hapo baadaye kwani hivi sasa hakuna nchi iliyoendelea ki soka bila kuanzia kwa vijana.
Mkisi amesema, hivi sasa vilabu vingi havina timu ya watoto ambao watakuzwa kisoka kuanzia chini hivyo kupelekea vilabu hivyo kuwa na wachezaji wengi ambao hawana mafunzo ya muda mrefu katika soka na kupelekea kushindwa kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.
Kwa upande wake Hababuu Ally ambaye pia ni kocha wa mpira wa miguu amesema, soka linashindwa kuendelea hapa nchini kutokana na kutokuwa na viongozi katika vilabu mbalimbali na hata maandalizi kwa timu sio ya kuridhisha na kuiwezesha timu kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.
Hababuu amesema, timu zimekuwa hazina maandalizi mazuri kwa kutokana na kutokuwa na viongozi na hata miundombinu ya kimichezo imekuwa sio ya kuridhisha kwa vilabu mbalimbali hapa nchini.





