
Msimamizi wa mpira wa kikapu kwa vijana Bahati Mgunda amesema ligi hii itachezwa kwa mfumo uleule unaotumika katika ligi ya NBA ya nchini Marekani ambapo kutakuwa na timu 30 huku kila timu ikiwa na wachezaji 15 na michuano hiyo itafanyika kila Ijumaa na Jumamosi kwa muda wa miezi tisa.
Mgunda amesema, watakuwa na wanafunzi 450 ambapo wanaamini programu hiyo itasaidia watoto kuwa na ndoto kubwa za kuweza kucheza ligi kubwa ya mpira wa kikapu duniani NBA.