Akizungumza na East Africa Radio Afisa Habari wa BMT Najaha Bakari amesema, wamependekeza kwa wenye vigezo vya kuwania uongozi wa chama hicho katika nafasi za makamu mwenyekiti, muweka hazina, Kamishna wa ufundishaji na njia za ufundishaji na kamishna wa ufukweni waendelee kujitokeza kabla ya kesho.
Najaha amesema, wanachama wanatakiwa kujitokeza kwa wingi Jumamosi ambayo ni siku ya Uchaguzi kwa ajili ya kupiga kura kwa kwa viongozi wanaowania nafasi mbalimbali katika chama hicho ili kuweza kuleta maendeleo ya mchezo huo hapa nchini.
