Tuesday , 7th Jun , 2016

Timu shiriki za michuano ya michezo ya Shule za Sekondari UMISETA Mkoa wa Dar es salaam zaahidi kurudisha heshima ya mkoa katika mashindano hayo.

Mlezi wa michuano ya UMISETA mkoa wa Dar as salama Celestine Mwangasi amesema,wanamatumaini makubwa ya kurudisha ushindi Mkoa wa Dar es salaam kutokana na taswira walioiyonyesha wanafunzi katika mashindano ya mkoa.

Mwangasi amesema, vijana wameonyesha vipaji cha hali ya juu katika mashindano ya mkoa yaliyopelekea hata wao kujiaminisha ya kuwa watafanya vizuri katika mashindano ya Taifa.

Mwangasi amesema, kumekuwa na changamoto nyingi katika mkoa wa Dar es salaam zilizopelekea mkoa kushindwa kuchukua ubingwa kwa upande wa mpira wa miguu kuanzia mwaka 2010.

Mwangasi amesema kwa maandalizi waliyoyafanya wanaamini watarudisha heshima katika soka la wanaune mkoa wa Dar es salaam.