
Uganda The Cranes
Kwa mujibu wa taarifa ya program za kocha mkuu wa timu ya Uganda, Milutin ‘Micho’ Sredejovic, timu itafanya mazoezi Tunisia na Dubai, katika kusaidia wachezaji kuzoea hali ya hewa ya unyevu unyevu.
Uganda Cranes tayari imeshabainisha kucheza mechi za kirafiki na Libya, Tunisia, Ivory Coast, huku pia ikifanya mazungumzo na Nigeria, juu ya kuwapata Super Eagles, kwa mchezo wa kirafiki.
Kikosi cha Uganda, kitakacho kwenda Gabon, Januari mwakani, kinatarajiwa kutangazwa na mwalimu Micho, Novemba 30, mwaka huu.