
Chama cha netball Tanzania CHANETA kimesema kuwa maandalizi ya michuano ya klabu bingwa kwa nchi za Afrika Mashariki inayotarajiwa kuanza Machi 22 mwaka huu jijini Dar es salaam yamekamilika kwa asilimia 85.
Hii leo CHANETA ilikua katika uwanja wa taifa kukagua viwanja vitakavyotumika katika michuano hiyo, ambapo mwenyekiti wa CHANETA Bi. Anna Kibira, amesema kuwa licha ya kuwa mpaka sasa hawajapata udhamini wanataraji kuendesha michuano hiyo kama ilivyopangwa
Aidha Kibira ameongeza kusema kuwa katika kuhakikisha timu za Tanzania zinafanya vema katika michuano hiyo ambayo itaanza march 22 mwaka huu hii leo wameandaa bonanza maalumu likishirikisha pia timu za netball za wanaume kwa lengo la kuhakikisha msimu huu kombe hilo linabaki kwa wanawake na wanaume kutwaa ubingwa.