Friday , 27th Nov , 2015

Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15 imeingia kambini kujiandaa na ziara ya mafunzo katika ukanda wa Afrika Mashariki itakayoanza Desemba Mosi Mwaka huu.

Kocha wa timu hiyo Sebastian Mkomwa amesema, vijana wote wameingia kambini na wameanza mazoezi kwa ajili ya mafunzo hayo ambapo mazoezi hayo yatafanyika mpaka siku ya safari.

Kikosi cha wachezaji 24 kimeingia kambini kujifua na ziara hiyo ambapo timu hiyo inaandaliwa kwa ajili ya kushiriki kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa ta Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwakani nchini Madagascar.