Monday , 23rd Feb , 2015

Vyama vya mikoa na wilaya vya kuogelea vimetakiwa kufanya uchaguzi wa viongozi kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Julai mwaka huu.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa Chama cha Kuogelea nchini TSA, Noel Kihunsi amesema, vyama hivyo vinatakiwa kufanya chaguzi ndogo ndogo na baada ya hapo watatakiwa kutuma majina ya viongozi hao pamoja na ada ili kuweza kushiriki uchaguzi mkuu.

Kihunsi amesema, lengo hasa la uchaguzi huo ni kuweza kupata viongozi wapya watakaoweza kukiendesha chama hicho na kuweza kuboresha na kukuza mchezo huo wa kuogelea hapa nchini.

Kihunsi amesema, iwapo mwanachama atakuwa hajakamilisha ada yake ndani ya miaka mitatu atakuwa amejifuta uanachama na hatoruhusiwa kushiriki shughuli zozote za chama. mkutano Mkuu wa Chama kuogelea nchini TSA unaotarajia kufanyika Aprili mwaka huu.