Mwenyekiti wa CHANETA Anna Kibira amesema, ili kupata nafasi ya kushiriki ni lazima timu zithibitishe mapema ili kutoa nafasi kwa chama chake kupeleka taarifa zao katika chama cha mchezo huo visiwani Zanzibar CHANEZA.
Kibira amesema, Klabu zinatakiwa kuthibitisha ushiriki wake kwa maandishi pamoja na kulipia baadhi ya gharama za ushiriki.
Mashindano ya ligi ya muungano kwa mwaka huu yanatarajiwa kufanyika Desemba saba visiwani Zanzibar huku Tanzania Bara ikitarajiwa kuwakilishwa na timu za uhamiaji, JKT Mbweni, Jeshi Stars, Mbeya City, Pilisi na Tumbaku za Morogoro.