Tuesday , 1st Jul , 2014

Chama cha mchezo wa Gofu nchini (TGU) kinatarajia kuanza kutoa mafunzo kwa shule mbalimbali hapa nchini ikiwa na lengo la kukuza mchezo huo

Mmoja wa wachezaji wa Gofu katika viwanja vya Lugalo

Chama cha mchezo wa Gofu nchini (TGU) kinatarajia kuanza kutoa mafunzo kwa shule mbalimbali hapa nchini ikiwa na lengo la kukuza mchezo huu katika shule mbalimbali hapa nchini.

Akizungumza na East Africa Radio,Mwalimu wa Gofu viwanja vya Lugalo Japhet Masai amesema mpango huo umeshaanza ambapo makamu mwenyekiti wa TGU Joseph Tango ameanza kwa kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa Makongo na baadhi ya wanafunzi hao wameshajisajili katika kambi ya Gofu ya Makongo kwa ajili ya kuanza rasmi mafunzo hayo.

Masai amesema ili kuendelea kukuza mchezo huu kwa vijana wameamua kuwashirikisha wanafunzi chipukizi katika mchezo huu katika maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambapo watashiriki kikamilifu katika mashindano ya Gofu yatakayofanyika Agosti 30 mapaka 31 mwaka huu viwanja vya Lugalo jijini Dar es salaam.