
Shirikisho la kandanda Tanzania TFF
Katika salamu hizo za rambirambi, TFF imewapa pole wafiwa, ndugu jamaa na marafiki na kusema wapo pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
Aidha pia TFF imetuma rambirambi (ubani) wa shilingi laki mbili (200,000) kwa familia ya kocha Hemed Moroco kufuatia kifo cha baba yake Suleiman Ally.
Mazishi ya marehemu Suleiman Ally Hemed imefanyika jana jioni mjini Zanzibar