Tuesday , 8th Dec , 2015

Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 inarejea jijini Dar es salaam baada ya ziara yake ukanda wa Afrika Mashariki kusitishwa kufuatia kukosekana kwa fedha ya kuihudumia baada ya TRA kufungia akauti za shirikisho la soka nchini TFF.

Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) ikikabidhiwa bendera ya Taifa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel katika hosteli za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam.

Akizungumza jijini Dar es salaam Afisa habari wa TFF Baraka kizuguto amesema ziara hiyo ya vijana ambao walikua waelekee katika nchi za Kenya,Rwanda na Uganda imedhaminiwa na shirikisho hilo jambo ambalo linashindwa kutekelezeka ktokana na fedha zote kuwa kwenye akaunti hizo.

Timu hiyo ya ilikua jijini Mwanza kucheza mechi za kirafiki inajiandaa na michuano ya mwakani ya kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 itakayopigwa nchini Madagascar mwaka 2017.

Hata hivyo Kizuguto amesema tayari jitihada zimeanza kufanyika ya kuhakikisha kila kitu kinakaa sawa ili kuruhusu shughuli za shirikisho hilo zinafanyika kama ilivyokusudiwa.

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA imezifungia akaunti zote za shirikisho hilo kwa kile kinachoelezwa ukwepaji wa kodi kinyume na sheria