Hayo yameelezwa na Afisa Habari wa TFF, Cliford Mario Ndimbo leo wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kusema golikipa huyo alidanganya umma alipokuwa anahojiwa baada ya kumaliza mchezo wao wa Kombe la Shirikisho la Azam ASFC uliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.
"Utaratibu wa TFF ni kuzipatia pesa timu kabla ya kucheza mechi zao utaratibu ambao umefanyika kwa Shupavu waliolipwa pesa zao jana ikiwemo na TFF kuwaongeza fedha ya ziada mara mbili zaidi kama yalivyokuwa maombi yao", alisema Cliford.
Kwa upande mwingine, Afisa Habari huyo amesema wanafanya utaratibu wa kumtaka Mgwira kuthibitisha madai yake na endapo atashindwa kuthibitisha ataadhibiwa kwa mujibu wa kanuni.

